RAIS WA MAREKANI DONALD TRUMP AMEMALIZA ZIARA YAKE YA WIKI MBILI BARANI ASIA

Rais wa marekani Donald Trump amemaliza ziara yake ya wiki mbili barani Asia kwa kuzungumza ana kwa ana na viongozi wa mataifa ya bara hilo huku akisisitiza zaidi kuhusu biashara na kitisho cha nyuklia cha Korea Kaskazini.
Viongozi kutoka nchi 10 wanachama wa jumuiya ya mataifa ya kusini mashariki mwa Asia Asean pamoja na China wamejadili kuepuka ugomvi katika eneo linalozozaniwa la bahari ya kusini mwa China katika mkutano wao unaofanyika nchini Ufilipino.
Trump amejitolea kuwa mpatanishi wa mzozo wa bahari ya kusini ya china inayowaniwa na mataifa sita ya kusini mwa asia, huku china ikisema itashirikiana na wenziwe kuutatua mzozo huo.
Nchi hizo mbili jirani na za kikoministi zimekuwa katika mvutano kuhusu bahari ambayo huwezesha biashara ya dola trilioni tano kila mwaka na ambayo inaaminika kuwa na utajiri mkubwa wa gesi.
Pia trump na mwenzake wa urusi vladimir putin wamekubaliana kuwa mzozo wa syria hauwezi kumalizwa kwa nguvu za kijeshi bali kisiasa, viongozi hao walitoa tamko la pamoja pembezoni mwa mkutano mkuu wa viongozi wa jumuiya ya ushirikiano wa kiuchumi wa nchi za asia na pacifiki (apec) nchini vietnam.