RAIS WA PERU PEDRO PABLO AMEMSAMEHE RAIS WA ZAMANI WA NCHI HIYO ALBERTO FUJIMORI

 

Rais wa Peru Pedro Pablo amemsamehe Rais wa zamani wa nchi hiyo alberto fujimori kwa kuzingatia hali yake ya kiafya, hatua ambayo imezua maandamano makali.

Fujimori, mwenye umri wa miaka 79, ambaye anatumikia kifungo cha miaka 25 jela kwa ukiukaji wa haki za binadamu na ufisadi, alihamishwa kutoka gerezani kwenda hospitalini kutokana na sababu za kiafya.

Rais pedro amekana kuwa kumsamehe kwake kulikuwa ni sehemu ya makubaliano ya chama chake kuzuia kura ya kutokuwa na imani naye.

Baada ya taarifa za hizo msamaha polisi katika mji mkuu wa lima wamepambana na waandamanaji waliokuwa wakipinga kuachiwa kwa fujimor.

Hata hivyo wafuasi wa fujimor ambaye aliongoza peru kuanzia mwaka 1990 hadi mwaka 2000 walisherehekea nje ya hospitali ya serikali aliyokuwa akipatiwa matibabu fujimor.