RAIS WA URUSI VLADIMIR PUTIN AMEIBUKA MSHINDI NA KULIONGOZA TAIFA HILO

Rais wa urusi vladimir putin ameibuka mshindi na kuliongoza taifa hilo kwa muhula mwingine ujao wa miaka sita baada ya kujipatia ushindi mkubwa.Ushindi huo ulitarajiwa katika upigaji kura uliomalizika  jumapili ambapo  kabla ya kura zote kuhesabiwa tayari putin alikuwa ameshajihakikishia  ushindi wa  asilimia 76 kwa mujibu wa tume ya uchaguzi nchini humo.Akizungumza katika mkutano wa kutangazwa mshindi putin, amesema ushindi wake ni matokeo ya hatua kubwa ya mafanikio aliyoyafikia katika uongozi wake.

Putin ameongeza kuwa huo ni uthibitisho wa kukubalika kwa sera zake na kwamba hana mpango wowote wa kufanya marekebisho ya katiba na kusisitiza umoja na mshikamano.akijibu maswali kutoka kwa waandishi wa habari  hata hivyo putin hakuweka bayana kwamba atagombea katika muhula ujao  wa uchaguzi ama laa.. ushindi huo mkubwa ambao ulitarajiwa,umekuwa na ongezeko la kura ikilinganishwa na ushindi wa asilimia 64 mwaka 2012.ambapo mpinzani wa karibu wa putin milionePavel grudinin,yeye alipata asimilia 12.