RAIS WA UTURUKI RECEP TAYYIP ERDOGAN YUPO MJINI DOHA

 

Rais wa Uturuki recep tayyip erdogan yupo mjini doha akifanya mazungumzo na Sheikh Tamim bin Hamad al Thani wa Qatar

Hii itakuwa ni ziara ya pili kwa kiongozi huyo wa Uturuki kwa nchi hiyo tangu kuzuka kwa mgogoro mkubwa wa kidiplomasia katika kanda hiyo ya ghuba miezi mitano iliyopita.

Erdogan pamoja na mambo mengine wanajadili kuhusiana na maendeleo ya kanda hiyo mikataba baina ya nchi hizo mbili ikiwa ni mwezi mmoja tokea viongozi hao wawili walipokutana katika mji mkuu wa uturuki ankara lakini suala la mgogoro huo litakuwa ajenda muhimu kwao.

Nchi za Saudi Arabia, Bahrain, umoja wa Falme za Kiarabu, na Egypt zimevunja mikataba na kuiwekea vikwazo Qatar june 5 kwa kuituhumu kuwa inaunga mkono ugaidi na kuendeleza mikataba na nchi ya iran madai yanayokanushwa na Qatar.

Erdogan amesema tangu kuzuka kwa mgogoro huo uturuki imekuwa ikizitaka pande zinazozozana  kufanya mazungumzo kwa kuweka tofauti zao pembeni ambapo amesema nchi hiyo iko upande wa qatar kwa kushirikiana katika masuala ya kijeshi jambo linalowakera nchi za upande wa pili katika mzozo huo.