RAIS WA ZAMANI WA BRAZIL AHUKUMIWA KIFUNGO JELA

RAIS WA ZAMANI WA BRAZIL AHUKUMIWA KIFUNGO JELA

Rais wa zamani wa Brazil Luiz Inacio lula da Silva amehukumiwa kifungo cha tisa na nusu jela kwa makosa ya rushwa na utakatishaji fedha haramu.

lula ni kiongozi wa ngazi ya juu kuhukumiwa katika uchunguzi wa rushwa ambao umesababisha kufungwa jela watu wengine kadhaa wa tabaka la juu katika nchi hiyo ya amerika kusini.

Rais huyo wa zamani amesema mashtaka hayo sio ya msingi kabisa na akaapa kugombea katika uchaguzi wa Rais mwaka ujao.

Rais huyo wa zamani atabaki huru wakati kesi yake ya rufaa ikisikilizwa.