RAIS WA ZAMANI WA ZIMBABWE ROBERT MUGABE ANARIPOTIWA KUWA KATIKA HALI MBAYA YA KIAFYA

 

Rais wa zamani wa zimbabwe Robert Mugabe mwenye umri wa miaka 94, anaripotiwa kuwa katika hali mbaya ya kiafya kiasi ya kwamba hawezi tena kutembea.

Rais wa zimbabwe emmerson mnangangwa amewaambia wafuasi wa chama tawala, kwamba mugabe amekuwa hospitali nchini singapore kwa miezi miwili anakopatiwa matibabu.

Katika taarifa yake hiyo ya jana, mnangagwa amesema mugabe alipanga kurudi zimbabwe oktoba 15 lakini kutoka na hali yake bado kuwa mbaya anatarajiwa kurudi novemba 30.

Mnangagwa hakutoa taarifa zaidi juu ya afya ya kiongozi huyo wa zamani.

Mugabe alikuwa kiongozi wa zimbabwe kabla ya kuondoshwa madarakani baada ya kuiongoza nchi hiyo kwa miaka 37.