RAIS WA ZANZIBAR DK ALI MOHD SHEIN AMEWATUNUKU NISHANI YA MAPINDUZI

Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dk Ali Mohd Shein amewatunuku Nishani    ya Mapinduzi, Utumishi uliotukuka na Nishani  Ushujaa watu 52 waliwahi kufanya kazi katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

hafla hiyo imefanyika  katika viwanja vya Ikulu  mjini  Zanzibar  ambapo waliotunikiwa waliowahi kuiletea sifa Zanzibar na kuonyesha maadili mema  ya kupigiwa mfano katika utendaji wa kazi

nishani hizo zimetolewa kwa waliokuwa wajumbe wa Baraza La Mapinduzi, makatibu wakuu, Wakurugenzi, watumishi wa idara maalum za smz  pamoja na   maafisa  na wapiganaji  wa vikosi vya ulinzi  na usalama wakiwemo wananchi  mabli mbali.

akitoa maelezo katibu mkuu ofisi ya Rais na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi ndugu Salum Hassan Salum amesema   nishani hizo zimekuja baada ya serikali kuridhirika na utendaji wa watu hao kutokana na kuchapakazi kwa uhodari.

amesema nishani hizo zimetolewa  kwa   watu walioasisi, kushiriki, kuyatukuza na kuyaenzi mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 na anaetunukiwa anatakiwa  kutumikia kwa muda usiopungua miaka 20 mfululizo  huku akionyesha tabia njema katika utumishi wake.

miongoni mwa watunukiwa nishani ni marehemu dkt Omar Ali Juma aliyawahikuwa waziri kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, marehemu Isaq Sepetu, makame mzee suleiman, Asha Bakari Makame na Hassana Haji Wambi Dk Omar Makame shauri

wengine ni Hamid Mahmoud Hamid aliyekuwa jaji mkuu Zanzibar, Aboud Talib Aboud, Mohamed Fakih alityekuwa katibu baraza la mapinduzi.