real madrid imepunguziwa adhabu ya kifungo cha kutokusajili

Klabu ya real madrid imepunguziwa adhabu ya kifungo cha kutokusajili wachezaji mpaka januari mwaka 2018 walichoadhibiwa na fifa. Madrid wamepunguziwa adhabu hiyo na mahakama ya usuluhishi michezoni (cas), hivyo timu hiyo inaruhusiwa kufanya usajili mwezi julai 2017. Mahakama hii ya usuluhishi michezoni, pia imeipunguzia madrid faini waliyotozwa kutoka pauni 282,000 mpaka pauni 188,000. Awali shirikisho la soka duniani fifa, liliifungia miamba hiyo ya soka la hispania kusajili wachezaji wapya mpaka mwaka 2018, baada ya kukiuka kanuni za usajili kwa wachezaji, chini ya umri wa miaka 18, adhabu kama hiyo washawahi kupewa mahasimu wao wa jadi barcelona.