REAL MADRID WAMEWEKA REKODI MPYA

 

Real madrid wameweka rekodi mpya baada ya kufuzu  fainali ya klabu bingwa bara ni ulaya  kwa mara ya 16, huku Zinedine Zidane akiwa kocha wa kwanza kufudhu kwenda fainali hizo mara 3 mfululizo baada ya Marcelo Lippi kwenye miaka 1996-1998.

Ilichukua Dakika ya 3 tu Joshua Kimmich aliwanyanyua kwenye viti mashabiki wa Bayern Munich baada ya goli la utangulizi, goli ambalo limemfanya Kimmich kuhusika katika mabao 7 ya Bayern Munich katika michuano  hiyo msimu huu(kafunga 4 na assist 3).

Goli la kusawazisha la dakika ya 11 la Karim Benzema limekuwa goli la pili msimu huu wa Ligi ya mabingwa  kufungwa baada ya kupigwa pasi nyingi(28), ni bao la Lucas Digne pekee ndilo ambalo zilipigwa pasi nyingi kuliko hili zikipigwa (29).

Karim Benzema  alifanikiwa kuongeza bao la pili kunako dakika ya 46 na hii ikiwa mara yake ya kwanza kufunga mabao 2 katika mechi moja ya Champions League tangu afanye hivyo mara ya mwisho mwaka 2014 dhidi ya Schalke 04 ya ujerumani.

James Rodriguez anaechezea kwa mkopo klabu ya baryen munich katika  dakika ya 63 aliufanya ubao wa matokeo kusomeka magogli 2-2 na sasa anakuwa mchezaji wa saba katika historia ya michuano hiyo ya vilabu barani ulaya kuwahi kuifungia pamoja na kuifunga Real Madrid. Real  Madrid sasa wanafuzu hatua hiyo ya fainali kwa magoli ya jumla 4-3  wakisubiri  mshindi kati ya Liverpool na As Roma kukutana katika fainali  huko mjini kiev.

Polisi jijini LIverpool wametoa ulinzi maalum kwa kumpa askari wa kumsindikiza nyota wa kikosi cha Liverpool, Mohamed Salah.

Salah raia wa Misri, pamoja na ulinzi wa timu alilazimika kuongezewa askari mmoja ambaye alimsindikiza yeye wakati kikosi hicho kikiingia kwenye uwanja wa ndege jijini hapo.

Liverpool ilikuwa inaondoka kwenda Italia kwa ajili ya mechi yao ya Ligi ya Mabingwa jijini Roma, Italia  dhidi ya AS Roma, usiku huu.

Salah aliongezewa askari kutokana na kiu ya mashabiki kutaka kupiga naye picha, jambo ambalo lilisababisha hali hiyo.

Majogoo hao wa  jiji la Liverpool wameonekana wakifanya mazoezi ya mwisho asubuhi ya leo katika kampeni yao ya kuhakikisha wanatinga fainali ya michuano hiyo ikiwa ni  miaka 13 imepita tangu kutwaa ubingwa huo  mwaka 2005 walipoifunga Ac Milan pia ya  ITALIA

Roma wataingia  katika dimba lao  stadio olimpico   wakiwa na kumbukumbu  ya kipigo cha magoli 5-2  walichokipata  uwanjani Anfield  katika mchezo wa kwanza

Hivyo watalazimika  kutumia juhudi na nguvu kubwa ili kupindua matokeo hayo  kama walivyofanya katika michezo yao ya mtoano hatua ya 16 bora dhidi ya shakhatar  Donetsk na ule wa robo  fainali dhidi ya mabingwa wa Hispania FC Barcelona.

Yote kwa yote ni dakika tisini za mchezo huo utakaoanza sa 3 dakika 45 usiku huu ndizo zitakazoamua mshindi atakaeweza kuungana na Real Madrid katika fainal ya mwaka huu huko jijini  kiev.