RIPOTI MAALUM YA UPOTEVU MKUBWA WA FEDHA ZA UMMA.

Serikali ya mapinduzi zanzibar imepokea ripoti maalum ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali iliyobainisha upotevu mkubwa wa fedha za umma.
Katika ripoti hiyo imebainika kuwa kuna tafauti kubwa baina ya fedha zinazotolewa na serikali kwa ajili ya mishahara ya watumishi wa umma na kiwango halisi kinachotumika kuwalipa na kwamba kuna pengo kubwa la upotevu wa fedha hizo.
Akizungumza na waandishi wa habari katibu mkuu kiongozi abdul-hamid yahya mzee amesema fedha hizo zimepotea kwa kuawalipa wafanyakazi ambao tayari wamestaafu, wafanyakazi waliochukua likizo bila malipo ambao hawastahili kulipwa na wale waliofikia umri wa kustaafu lakini bado wanaendelea na utumishi wa umma na kulipwa.
Amesema serikali inafanya uchunguzi wa kina dhidi ya wale wote waliochukua fedha za umma kinyume na utaratibu na endapo ikithibitika hatua za kinidhamu na kisheria zitachukuliwa dhidi yao huku akizitaja baadhi ya wizara ambazo zimebainika na tatizo hilo kuwa ni wizara ya elimu na mafunzo ya amali, wizara ya afya, na wizara ya kilimo maliasili na uvuvi.
Amezitaja hatua za awali ambazo zinakusudiwa kuchukuliwa na serikali ni pamoja na kufanya uhakiki kwa wanafuzi walionda kusoma kwa muda mrefu na hawajarudi katika maeneo yao ya kazi, kufanywa uhakiki kwa watumishi wagonjwa wa muda mrefu pamoja na waliofikia umri wa kustaafu kustaafishwa kwa mujibu wa sheria.
Ukaguzi hiyo ya ukaguzi imefanyika katika kipindi cha miezi sita kuanzia june hadi novemba 2016.