RIPOTI YA HAKI ZA BINADAMU ZANZIBAR IMEZINDULIWA HUKU IKIBAINISHA CHANGAMOTO

Ripoti ya haki za binadamu zanzibar imezinduliwa huku ikibainisha changamoto nyingi ikiwemo ongezeko la vitendo vya uvunjaji wa haki hizo.

ripoti hiyo imetaja kuwa katika mwaka 2016 matukio ya ajali za barabarani pekee yamesababisha vifo vya watu 155 na majeruhi kadhaa ikilinganishwa na mwaka 2015 ambapo watu 150 walifariki chanzo kikubwa ikiwa ni uzembe katika matumizi ya barabara.

akiwasilisha ripoti hiyo msimamizi wa dawati la haki za binadamu kutoka kituo cha huduma za sheria zanzibar Thabit Abdalla Juma amesema matukio mengine ya uvunjifu wa haki za binadamu yaliyojitokeza ni pamoja na mauwaji huku matukio 34 yameripotiwa katika vituo mbalimbali vya polisi.

hata hivyo thabit amesema ripoti imeonyesha kuwa kuna mafanikio yaliyofikiwa katika sekta ya aelimu ambapo idadi ya waliopatiwa mikopo kwa ajili ya masomo ya elimu ya juu imeongezeka na kupunguza tatizo la ucheleweshwaji wa kesi mahakamani.

akizindua ripoti hiyo mwenyekiti wa tume ya kurekebisha sheria Zanzibar Jaji Mshibe Ali Bakari amesema kutokana na malalamiko mengi juu ya suala la haki za binadamu ameomba kuongezwa ushirikiano kati ya jamii na amewahimiza watendaji wa sheria kuondosha urasimu katika kutenda haki.

ripoti hiyo ya kumi na moja imetolewa na kituo cha huduma za sheria zanzibar.