RIPOTI YA PILI YA KILA MWAKA KUHUSIANA NA HALI YA HAKI ZA BINADAMU

 

Taasisi ya haki za binadamu nchini ujerumani imetoa ripoti ya pili ya kila mwaka kuhusiana na hali ya haki za binadamu nchini ujerumani, ikisema kwamba mamia kwa maelfu ya wahamiaji nchini humo wanakabiliwa na changamoto za kuishi katika mazingira duni, kupata taabu kujumuika katika nchi yao mpya na pia wanakabiliwa na unyanyasaji.

Mkurugenzi wa taasisi hiyo, beate rudolf, amesema  kwamba kuna upungufu kwa waombaji hifadhi laki nne nchini ujerumani lakini ripoti kamili inatarajiwa kuwasilishwa desemba 10 katika siku ya kimataifa ya haki za binadamu katika bunge la ujerumani.