Riyad Mahrez ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa afrika

Kiungo wa Leicester city Riyad Mahrez ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa Afrika wa mwaka. Mahrez mwenye Umri wa miaka 25 raia wa Algeria aliyeisaidia Leicester kushinda taji la ligi kuu ya Uingereza msimu uliopita, tayari ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa England sambamba na mchezaji bora wa BBC Afrika. Mshambuliaji wa Senegal na klabu ya Liverpool Sadio Mane na mshambuliaji wa Borussia Dortmund na timu ya taifa ya Gabon Pierre-Emerick Aubameyang walikuwa wakiwania tuzo hiyo. Mshambuliaji wa Arsenal na timu ya taifa ya Nigeria Alex Iwobi ameshinda tuzo ya mchezaji bora chipukizi. Denis Onyango wa uganda na klabu ya Memelodi Sundowns ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa ligi za ndani. Mchezaji bora kwa kina dada imenyakuliwa na Asisat Oshoala wa Liverpool na timu ya taifa ya Nigeria huku timu bora ya mwaka ikiwa ni Uganda