SAMAKI AINA YA CHEWA SOKO KUBWA NA KUONGEZA KIPATO KWA WAVUVI

 

Samaki aina ya chewa  wanaovuliwa hapa nchini  katika msimu wa kiangazi  wameonekana kuwa na soko kubwa na kuongeza kipto kwa wavuvi na taifa kwa ujumla.

Samaki hao  huvuliwa zaidi  katika mwambao wa ukanda wa  bahari ya kizimkazi na   mtende ambapo mafanikio  makubwa  yamekuwa yakipatikna kwa wakazi wa vijiji hivyo .

zbc ilipata fursa ya kuzungumza na  mvuvi mashuhuri wa samaki  wakubwa  wakiwemo chewa  papa  jodari  na mbase badru simai  amesema umakini zaidi unahitajika wakati wa kuwavua samaki hao ambao wamekuwa na uwezo mkubwa na nguvu zaidi na hupatikana  kina kirefu cha maji kati yamita  55 hadi 90

Amefahamisha kuwa  mwishoni mwa wiki iliyopita   kijiji cha   kizimkazi  dimbani  kilifanikiwa kuvua chewa  mkubwa  mwenye urefu wa sentimita 223  na  110 na upana ni sentimita 95 na 85 ambapo walikadiriwa kuuzwa kwa zaid ya shilingi milioni moja tz

Amesema mafanikio  hayo yanatokana na kuimarika  kwa uchumi hasa katika sekta ya uvuvi huku akiwasihi wavuvi wezake  kuzitunza rasilimali za bahari zilizopo  nchini .