SAUDI ARABIA KURUHUSU MISAADA YA KIUTU KUINGIA NCHINI YEMEN

 

Rais donald trump wa marekani ameitaka saudi arabia kuruhusu  misaada ya kiutu kuingia nchini yemen ,  ikiwemo chakula, mafuta, maji na dawa kuwafikia watu zaidi ya milioni 7 nchini humo ambao umoja wa mataifa unasema wako katika hatari ya kukabiliwa na njaa.

Lakini trump hakutoa ombi la kusitishwa kabisa kwa mashambulizi yanayofanywa na majeshi ya muungano yanayoongozwa na saudi arabia, hali inayoelezwa na umoja wa mataifa kuwa moja kati ya mzozo mkubwa kabisa wa kibinadamu.

Mapigano mjini sanaa yameongezeka kati ya waasi wa kihuthi na majeshi ya serikali baada ya rais wa zamani wa yemen ali abdullah saleh kuuwawa siku ya jumatatu.

Saudi arabia na washirika wake wameanzisha kampeni ya kuwaondoa waasi wa kihuthi ambao wanadhibiti mji mkuu sanaa.