SAUDI ARABIA YANAENDELEZA MASHAMBULIZI KUIRUDISHA BANDARI MUHIMU

 

Majeshi yanayoungwa mkono na saudi arabia yanaendeleza mashambulizi ya kutaka kuirudisha bandari muhimu inayodhibitiwa na waasi ya hodeida nchini yemen, huku juhudi za umoja wa mataifa za kusimamisha mapigano nchini humo zikionekana kuzorota na kusababisha wasiwasi kwa raia.

Baada ya wiki mbili za mazungumzo katika mji mkuu wa yemen, sanaa, mjumbe wa umoja wa mataifa martin griffith ametoa taarifa fupi mbele ya baraza la usalama la umoja wa mataifa kuhusiana na juhudi za kumaliza mzozo dhidi ya bandari hiyo muhimu inayotumika kuingizwa misaada kwa raia wa yemen, wanaokabiliwa na njaa.

Hata hivyo baada ya mazungumzo na griffith  waasi wa houthi wanaoungwa mkono na iran wamesema mazungumzo hayo yameshindwa, na hakuna makubaliano yaliyofikiwa, huku kiongozi wa serikali yao isiyo rasmi akipinga usitishaji wa mapigano chini ya masharti ya sasa .