SAUDIA ARABIA UMEKABIDHI ZANZIBAR SADAKA YA NYAMA TANI 150

 

ubalozi wa Saudia Arabia umekabidhi sadaka ya nyama tani 150 yenye thamani ya zaidi ya shilingi zaidi ya shilingi milioni mia tatu na sabini kwa kamisheni ya wakfu na mali ya amana zanzibar.

Akikabidhi sadaka hiyo kaimu balozi wa saudi arabia tanzania bw nayif jadii amesema zanzibar imekuwa ikifanya vyema katika kutoa sadaka hizo kwa wahusika kutokana na utaratibu huo nchi yake  imeamua kuongeza sadaka hiyo kwa mwaka huu ili iweze kuwafikia waumini wengi zaidi hasa wale wenye hali ya chini.
Akipokea sadaka hiyo, waziri wa nchi ofisi ya rais katiba, sheria utumishi wa umma na utawala bora mhe, haroun ali suleiman amefurahishwa na msaada huo  na kusema msaada huo una lengo la kuimarisha  mashirikiano yaliyopo kati ya zanzibar na serikali ya saudia.
Mapema katibu mtendaji wa kamisheni ya wakfu na mali ya amana shekh abdalla talib amesema tayari nyama itagaiwa kwa wahusika ambapo kati ya kontena nne zilizopokelewa mbili zitapelekwa pemba na mbili unguja