SAUTI MOJA KATIKA KUSIMAMIA MALEZI NA MIENENDO YA WATOTO YA KILA SIKU.

 

Mafanikio dhidi  ya   vitendo   vya  udhalilishaji   yatapatikana    iwapo   familia  zitakuwa  na   sauti   moja   katika  kusimamia    malezi  na   mienendo   ya  watoto  ya  kila  siku.

Naibu  katibu mkuu  wa   wizara  ya  uwezeshaji  wanawake  wazee   vijana  na  watoto  nd  hassan  khatibu     amesema  hayo  katika   uzinduzi  wa  baraza  la  malezi   kichama  wilaya  dimani  amesisitiza    umuhimu  wa   kukemewa  vikali  vitendo  hivyo   kutokana  na kuifedhehesha    familia  sambamba  na  kumuathiri   kisaikolo jia mtendewa.

Mkurugenzi  wa   idara  ya  wanawake  na  watoto nd  nasima  haji  choum  amesema  wizara  ipo  pamoja  na  jamii  katika  kurudisha  malezi  yenye  maadili   ili  kuendelea  kudumisha  silka  na  utamaduni  wa  malezi  ya  pamoja.

Katibu  wa  jumuiya  wazazi  wilaya  dimani  nd makame   yusuf  amesema  lengo  la  baraza  hilo  ni   kutekeleza  kuhakikisha  watoto  wanalelewa  katika  maadili  na   mazingira    salama .