SEKTA BINAFSI ZIMETAKIWA KUITUMIA FURSA WALIYOPEWA NA SERIKALI

sekta binafsi zimetakiwa kuitumia fursa waliyopewa na serikali ya kushirikiana kwa pamoja katika kuwapatia wajasiriamali mbinu mbadala na za kisasa za uzalishaji wa bidhaa zinazokwenda na wakati ili kupunguza tatizo la ajira hasa kwa vijana.
wito huo umetolewa ukumbi wa jamuhuri wete na katibu tawala wa mkoa wa kaskazini pemba ahmed khalid abdalla kwa niaba ya mkuu wa mkoa huo wakati akifungua mafunzo ya kijani kibichi kwa wajasiriamali na vijana, yaliyoandaliwa na jumuiya ya maendeleo ya elimu zanzibar (zedo).
katika hotuba hiyo katibu ahmed amesema uzalishaji wa bidhaa za wajasiriamali zinachangia uchumi wa nchi, hivyo sekta binafsi zinapaswa kusimamia bidhaa hizo kwa lengo la kuwakombowa wananchi hasa vijana ambao wanategemea zaidi kuajiriwa serikalini.
akizungumzia suala la haki ya msingi ya elimu katibu huyo ameishuri jumuiya ya zedo kutanua wigo wa kutembelea maeneo ya bandarini ili kuwashawishi watoto na vijana walioacha skuli kuwarejesha ili waendelee na masomo yao.
akelezea lengo la mafunzo hayo mweneyekiti wa jumuiya ya zedo ussi said suleiman ameipongeza serikali kwa kuingiza masomo ya ujasiriamali katika mitaala ya ufundishaji, kwani vijana wakipata mafunzo hayo mapema watajenga mawazo ya kujiajiri wenyewe