SEKTA BINAFSI ZINAMCHANGO MKUBWA KATIKA KUISAIDIA SERIKALI KUTOA HUDUMA TOFAUTI

Waziri wa afya Hamad Rashid Mohammed amesema sekta binafsi zinamchango mkubwa katika kuisaidia serikali kutoa huduma tofauti ikiwemo huduma ya afya .

Kauli hiyo ameitoa wakati akifungua hospital ya urban pamoja na kuzindua bonaza la uchangiaji damu na kueleza kuwa hospitali hiyo itasaidia kutoa huduma za afya kwa wakaazi wa maeneo hayo na jirani pamoja na wageni wanaofika nchini.

Akizungumzia kuhusu huduma ya uchangiaji wa damu kwa hiyari Mh: Hamad amesema ni vyema wananchi kuchangia damu na kuweza kuwa na akiba ya kutosha ili kuepukana na usumbufu katika mwezi mtukufu wa ramadhani.

Kwa upande wake mkurugenzi wa urban hospital Dk. Jane amesema watendelea jitihada ya kunga mkono serikali ya Zanzibar hasa katika sekta ya afya ili iweze kuimarika pamoja na kuwahamasisha wageni na wenyeji kuchangia damu.

Nae msaidizi meneja wa benk ya damu salama Zanzibar Magarawa amesema lengo ni kupata chupa 2000 kwa kipindi cha mwezi mtukufu wa radhamani ambayo itawasaidia kuwahudumikia wananchi ambao wanahitaji huduma hiyo.

Wakati huo huo waziri Hamad amepokea cheki ya millioni tatu kutoka shirika la bima la taifa tanzazni kwa ajili ya bonaza la kuchangia damu.

Comments are closed.

Powered by Live Score & Live Score App