SEKTA YA ELIMU INAWEZA KUIMARIKA ZAIDI IWAPO KUTAKUWA NA MIKAKATI YA PAMOJA

Sekta ya elimu katika mkoa wa kusini unguja inaweza kuimarika zaidi iwapo kutakuwa na mikakati ya pamoja katika utekelezaji wa mpango wa madarak mikoani maarufu kama ugatuzi.
Mkurugenzi wa halmashauri wilaya ya kati ndugu moh.d salum amesema mikakati hiyo itaimarika iwapo maafisa wa elimu na walimu wakuu wa skuli za mkoa huo watakuwa tayari kuifahamu dhana hiyo katika kurahisisha maendeleo kuanzia ngazi za chini ya jamii.
Akizungumza viongozi hao katika mafunzo elelekezi kuhusu mpango wa sekta ya elimu kuingizwa katika serikali za mitaa amewaomba kushirikiana ili kusaidia kutatua changamoto zinzowakabili katika kazi zao.
Akiwasilisha mada kuhusu serikali za mitaa mkurugenzi mipango, sera na utafiti ofisi ya rais tawala za mikoa daima mohamed mkalimoto amesema lengo la mpango huo ni kurahisisha upatikanaji wa huduma za kijamii na kuleta usawa kwa wananchi.
Wakichangia mkutano huo baadhi ya washiriki wameomba kutolewa elimu zaidi kwa jamii ili kuunga mkono mabadiliko hayo hasa sekta ya elimu.