SEKTA YA KILIMO KUCHANGIA PATO LA TAIFA

 

Uimarishwaji wa sekta ya kilimo ni moja ya mkakati wa chama cha mapinduzi ya kuifanya sekta hiyo kuchangia pato la taifa kwa zaidi ya asilimia 30.

Mjumbe wa baraza kuu la wazazi taifa shaabn khamis haji amesema mkakati huo pia umelenga kuongeza maeneo ya kilimo kufikia laki mbili ili kuwawezesha wakulima kulima kwa faida na kuongeza pato hilo ambapo kwa sasasekta ya kilimo inachangia uchumi kwa asilimia 31.

Akizungumza katika wiki ya kuelekea maadhimisho ya miaka 47 ya jumuiya ya wazazi kwa kushiriki kazi za upaliliaji mpunga katika shamba linalosimamiwa na kikundi cha uzalishaji cha jumuiya ya wazazi huko cheju amesema katika kufikia azma hiyo serikali imepanga kuweka mabwana na mabibi shamba kila shehia ili kuwasaidia wakulima.

Kwa upande wa wanakikundi wamesema wamejipanga kulima ekari tano katika kipindi kijacho kutoka ekari mbili wanazolima hivi sasa lakini wameomba kusaidiwa kutatuliwa masuala muhimu ili kufika lengo hilo.

Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi mkoa wa kusini ungujand. Juma suleiman khamis  amesema jumuiya itakuwa karibu kusaidia juhudi za kukuza uchumi kama inavyoelekeza ilani ya ccm.