SEREKALI YA JAMUHURI YA WATU WA CHINA IMETILIANA SAINI MAKUBALINO YA AWALI NA HOSPITAL YA ABDALLA MZEE

 

Serekali ya Jamuhuri ya watu wa china kupitia  timu ya madaktari kutoka jimbo la jiansu imetiliana saini makubalino ya awali na hospital ya abdalla mzee juu ya uanzishwaji wa kituo cha mafunzo  ya matibabu ya mifupa kwa madaktari wa fani hiyo Unguja na Pemba yatakayofanyika katika hospital hiyo kuanzia mwakani.

Katika makubaliano hayo ya awali,  kwa upande wa timu ya madaktari kutoka  china saini hiyo imekwa na Dr. Chen er jong ambapo kwa upande wa hospitali ya rufaa ya Abdalla mzee imewekwa na mganga mkuu dk. Haji mwita haji,  katika hafla ya kusherehekea kutumia mwaka mmoja tokea kufunguliwa upya kwa hospitali hiyo tarehe 26 novemba 2016.

Akitoa maelezo juu ya uanzishwaji wa mafunzo hayo Dr. Chen amesema serekali yao imekuwa ikichangia vitu mbali mbali katika hospitali hiyo ili kuunga mkono juhudi za serekali ya mapinduzi ya zanzibar ya kuwapatia matibabu bora wananchi wake.

Akitoa nasaha zake mkuu wa wilaya ya mkaoni hemed suleiman abdalla ameahidi kutoa ushirikiano kwa hospital hiyo katika utowaji wa mafunzo hayo ili madaktari wetu waweze  kupata ujuzi utakawasaidia kutoa huduma bora na kwa uhakika.

Wakimkaribisha mkuu wa wilaya katika hafla hiyo, mganga mkuu wa hospital ya rufaa ya Abdalla mzee Dr haji mwita haji na mkuu wa idara ya uendeshaji wa huduma za hospitali pemba Dk. Yussuf wamesema kuwa  asilimia  hamsini 50% ya bajeti  inaelekezwa katika  hospitali hiyo ili kutatua changamoto za utowaji wa huduma

Hospitali ya abdalla mzee imefunguliwa upya na raisi wa zanzibar  dr ali mohamed shein tarehe 26 november 2016 baada ya kufanyiwa matengenezo makubwa ya majengo pamoja na uwekaji wa viafaa vya kisasa kupitia serekali ya jamuhuri ya watu wa china ambapo leo imetimiza mwaka mmoja tokea kufunguliwa huko: