SEREKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR IMESEMA IMEFANYA UGATUZI KWA BAADHI YA WIZARA ZAKE

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema imefanya Ugatuzi kwa baadhi ya Wizara zake ili kutoa fursa kwa wizara hizo kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.

hayo yamebainishwa katika mikutano maalum ya kuhamasisha mikutano kwa walengwa wa mpango wa Ugatuzi katika mikoa ya kusini na kaskazini Pemba inayoendeshwa na wizara ya nchi ofisi ya Rais Tawala za mikoa Serikali za mitaa na idara maalum za SMZ

Serikali ya mapinduzi ya zanzibar imesema imefanya ugatuzi kwa baadhi ya wizara zake lengo ili kutoa fursa kwa wizara hizo kufamnya kazi kwa ufanisi zaidi

naibu katibu mkuu ofisi ya Rais tawala za mikoa Serikali za mitaa na idara maalum za SMZ Kai Mbarouk amesema Serikali imeamuwa kufanya ugatuzi huo ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za kijamii na kujenga uhusiano mwema baina ya watumishi wa umaa na wananchi

hayo yamebainishwa katika mikutano maalum iliyofanyika kwa nyakati tofauti katika mikutano na walengwa wa ugatuzi huo katika mikoa ya kusini na kaskazini Pemba.

akizungumza na walimu na wahudumu wa afya katika mkoa wa kasikazini pemba naibu waziri ofisi ya rais tawala za mikoa serekali za mitaa na idara maalum za SMZ shamata shaame khamis amesema serekali haina lengo la kuwakomoa wananchi bali nikutaka kuona kunakuwa na  ushirikiano wa pamoja na  kuleta ufanisi zaidi katika mamlaka zao

akitowa maada juu ya Ugatuzi huo Mkurugezi Mipango Sera na Utafiti Naima Mohammed Mkali Moto amesema zoezi la Ugatuzi lina lengo la kuleta madaraka karibu na jamii kuharakisha maendeleo husika miongoni mwao

nao baadhi ya wadau katika mikutano hiyo wamezitaka wizara husika wanatoa stahiki kwa wafanyakazi wao kwa wakati ikiwemo pesa za likizo.

wizara zilizofanyiwa ugatuzi huo  ni pamoja na elimu afya na kilimo