SEREKALI YA SMZ ITAENDELEA KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA MIJINI NA VIJIJINI

Waziri wa afya MH Mahamoud Thabit Kombo amesema serekali ya smz itaendelea kuboresha huduma za afya kwa wananchi wake mijini na vijijini
Waziri mahamoud ameyaeleza hayo katika ziara yake ya kuangalia shughuli za ujenzi zinavyo endelea katika vituo vya afya wilaya ya kati pamoja wilaya ya kaskazini ‘a’
Amsema serekali ya mapinduzi ya zanzibar chini ya uongozi wa dk ali moh’d sheni imedhamiria kuimarisha sekta ya afya nchini kwaajili ukwaondoshea wananchi usumbufu kuzifata huduma mbali na maeneo yao.
Mkuu wa wilaya ya kati mashavu sukwa ameipongeza serikali kupitia wizara ya afya kwa kuzitanuwa huduma za afya katika wilaya yake kwa kuwaekea vituo vitano ambavyo vitasaidia kupunguza msongamano katika hospital za rufaa.
Kwa upande wake dr fadhili muhammed abdallah mkurugenzi kinga na elimu ya afya zanzibar amewataka wananchi wenyewe kuibeba sekta ya afya pamoja na kushikiana na waunguzi katika kuvitunza vituo hivyo vilivyo katika maeneo yao.
Kwaupande wao wananchi wa kijini na chaani kikobeni wameishukuru serikali kwa kuitanua huduma hiyo katika ngazi za chini zai
Katika ziara hiyo ilioanza kiboje,urowa ,kijini,na kumalizia chaani kikobweni. Mradi huo ulio shirikiana serikali ya smz na orio.