SERIKALI HAITAIFUMBIA MACHO ANAEHATARISHA MAISHA YA RAIA WASIOKUWA NA HATIA

Naibu waziri wa mambo ya ndani ya nchi mhandisi hamad yussuf masauni amesema serikali haitaifumbia macho raia au mgeni anaehatarisha maisha ya raia wasiokuwa na hatia na amewaomba wananchi kusaidia kupambana na hali hiyo katika maeneo yao.
Masauni ameyasema hayo alipokuwa katika ziara yake ya kuhamasisha ujenzi wa vituo vya polisi katika maeneo ya mbande na tuangoma, wilayani temeke jijini dar es salaam.

Kwa upande wake kamanda wa polisi mkoa wa kipolisi temeke kamishna msaidizi mwandamizi wa polisi sacp gilles mroto ametoa rai kwa watendaji wa serikali za mitaa kuhakikisha wanakuwa na daftari la wakazi katika maeneo yao na kuepuka kuwapangisha nyumba madalali bila ya kumuona mpangaji.
Wananchi wa maeneo hayo wamezungumzia changamoto wanazokumbana nazo katika suala zima la ulinzi na usalama.