SERIKALI HAITAMVUMILIA MTU YEYOTE ATAKAE HARIBU VIANZIO VYA MAJI

 

Mkuu wa wilaya ya magharibi  A  Kepten Khatib Khamis Mwadini amesema serikali haitamvumilia mtu yeyote atakae haribu vianzio vya maji na kuwakosesha wananchi  kupata huduma hiyo

Akizungumza  wakati  wa zoezi la usambazaji wa mabomba na uwekaji wa matenki ya maji  katika kisima cha  shehia ya mwakaje

Amesema  wapo baadhi ya  watu ambao wamekuwa wakirejesha nyuma juhudi za serikali katika kuwaletea maendeleo wananchi wake kwa kuharibu miundombinu ya maji  kwa makusudi hivyo amewataka kuacha mara moja vitendo hivyo

Kepten khatibu  amewapongeza viongozi wa jimbo la mfenesini kwa juhudi kubwa za kuwatumikia wananchi na kutekeleza ilani ya ccm   huku akiwataka  wananchi  kuthamni juhudi za viongozi wa jimbo hilo  katika miradi mbalimbali ya maendeleo wanayoitekeleza

Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Mfenesini Kanal Mstaafu Masoud Khamis amesema  hadi sasa wamefanikiwa kuchimba visima zaidi ya kumi  katika jimbo hilo na kuweza kupunguza  changamoto kubwa ya huduma ya maji safi na salama iliyokuwa ikiwakabili wananchi wa jimbo hilo kwa muda mrefu na kulazimika kufuata masafa marefu

Nao baadhi ya wananchi walioshiriki zoezi  la ulazaji mindo mbinu ya maji  wamewashukuru viongozi wa jimbo lao kwa kutimiza ahadi za kuwapatia maendeleo kwa haraka