SERIKALI HAITOKUWA TAYARI KUONA WATU WANAFANYA VITENDO VYA HATARI

makamu wa pili wa rais wa zanzibar balozi seif ali iddi amesema serikali haitokuwa tayari kuona baadhi ya watu wanafanya vitendo vya hatari vinavyotishia maisha ya wananchi pamoja na wageni wanaoingia nchini.
amesema vyombo vya dola vitaendelea kudhibiti hali hiyo ili kutoa fursa kwa wananchi na wageni hao hasa wale wanaoingia nchini kwa shughuli za kitalii kufanya mambo yao katika misingi ya amani na utulivu.
balozi seif ali iddi alitoa kauli hiyo kwa nyakati tofauti wakati alipowatembelea bibi jennifer wolf raia wa ujerumani mwenye umri wa miaka 24 hapo kwenye makaazi yao mbweni aliyejeruhiwa kichwani kwa kuchomwa kisu na bwana mauget gerarol raia wa ufaransa mwenye umri wa miaka 66 aliyejeruhiwa jicho na kulazwa hospitali ya global mnazi mmoja.
hata hivyo raia huyo wa ufaransa bwana gerarol ameamuliwa kupelekwa jiji dar es salaam kwa matibabu zaidi wakati wenzao wengine anna catharina miaka 20 raia wa ujerumani, liying liang raia wa canada, hassan abdulla abdulla wa kiponda na sajad hussein wa mkunazini walipata matibabu na kurudi nyumbani kufuatia mkasa uliowakumba wakati wakipata huduma za chakula juzi usiku katika mkahawa la loukman mkunazini.
balozi seif akiwafariji majeruhi hao alisema ni jambo la kusikitisha kuona baadhi ya watu wanaamua kuhatarisha maisha ya wenzao bila ya sababu za msingi jambo ambalo vyombo vya ulinzi vitapambana nayo kwa nguvu zote.
aliwataka waathirika wa tukio hilo la kusikitisha kuwa na moyo wa subra wakielewa kwamba mitihani ni mambo wanayopambanao nayo wanaadamu katika shughuli na harakati zao za kimaisha za kila siku.
alisema yapo matukio ya kuhatarisha maisha ya watu yanayotokea na kuripotiwa na vyombo mbali mbali vya habari katika sehemu mbali mbali duiniani yakihusisha utashi wa mtu bila ya kuzingatia athari inayoweza kuikumba jamii inayozunguuka maeneo husika.
akielezea mikakati iliyowekwa na jeshi la polisi katika kupambana na vitendo vya kihuni na kuhatarisha maisha ya raia kamanda wa polisi mkoa mjini magharibi kamishna msaidizi muandamizi wa polisi hassan nassir ali alisema tukio hilo ni uhalifu wa kaiwaida uliowakumba sio wageni pekee bali hata watu wengine waliokuwepo sehemu hiyo.
kamanda nassir alisema jeshi la polisi limeshabaini mtuhumiwa wa tukio hilo ni kijana anayejihusisha na utumiaji wa dawa za kulevya lakini bado anaendelea kufuatiliwa ili atiwe mikononi kwa ajili ya kujibu makosa yanayomkabili.
mapema balozi mdogo wa shirikisho la ujerumani aliyepo zanzibar bwana dominic wolf pamoja na mke wa mjeruhiwa wa kifaransa bibi makhtin mauget wameishukuru serikali ya mapinduzi ya zanzibar kupitia vyombo vyake vya ulinzi kwa hatua ilizochukua kukabiliana na tukio hilo.
bwana dominic na bibi makhtin walisema wao pamoja na majeruhi wao wamepata faraja kubwa iliyowapa matumaini ya kuendelea kuwa mawazo ya kutaka kuityembelea tanzania na zanzibar kwa ujumla.