SERIKALI HAITOMFUMBIA MACHO MTU ATAKAE BAINIKA KUSHIRIKI KATIKA KUSULUHISHA KESI ZA UDHALILISHAJI

Serikali ya mapinduzi ya zanzibar imesema haitomfumbia macho mtu yoyote atakae bainika kushiriki katika kusuluhisha kesi za udhalilishaji wa wanawake na wanawake.
Naibu waziri kazi uwezeshaji wazee vijana wanawake na watoto mh. Shadya mohamed suleimana amesema serikali inamaliza mpango wa kuandaa taratibu za kisheria ili kuwapandisha mahakamani wato hao ambao wanachangia ongezeko la vitendo hivyo.
Mh. Shadya amesema hayo katika kijiji cha majinga shehia ya kiungoni alipoitembelea famulia ya siti ali fakih kwa lengo la kumpa pole kufuatilia watoto wake watatu kudhalilishwa huku mmoja akiwa na ujauzito.
Akielezea tukio hilo sheha wa kiungoni na afisa ustawi wa jamii wilaya ya wete haroub suleiman amesema wanaendelea kulifuatilia tukio hilo katika vyombo vya sheria na kubainisha kwamba jamii ya eneo hilo bado inatawaliwa na muhali katika vitendo hivyo.
Wakati huo huo naibu shadya alionana na kamanda wa poilisi mkoa wa kaskazini pemba haji khamis kujua namna kesi hiyo inavyoendelea.