SERIKALI HAITOMVUMILIA MTENDAJI YEYOTE ATAKAEKWENDA KINYUME NA MAADILI YA KAZI

Serikali ya mapinduzi zanzibar imesema haitomvumilia mtendaji yoyote atakaekwenda kinyume na maadili ya kazi katika kusimamia suala la udhalilishaji.
Akisoma hotuba ripoti ya ufafanuzi wa ushauri uliotolewa na kamati ya maendeleo, wanawake, habari na utalii, waziri wa wizara ya kazi uwezeshaji wazee vijana wanawake na watoto, mh. Moudline castico amesema serikali itahakikikisha inaweka mifumo imara ya kuondosha mianya inayozorotesha ikiwa ni pamoja na kuzifanyia marekebisho sheria zilizopitwa na wakati.
Amesema wizara hiyo imeanzisha operesheni maalum ya kusimamia kesi za udhalilishaji ambapo jumla ya kesi 139 zimesikilizwa.
Akiwasilisha hotuba ya maoni ya kamati mjumbe wa kamati hiyo mh. Maryam thani, ameishauri wizara kupitia taasisi zote zinazoshughulikia masuala ya udhalilishaji kuzidisha ushirikiano ili kutokomeza kabisa vitendo hivyo.
Aidha kamati hiyo imeitaka jamii kuwa waangalifu juu ya mialiko ya sherhe wanayopewa hasa watoto kwani miongoni mwa mialiko hiyo mambo yanayofanywa sio mazuri katika jamii.
Wakichangia hotuba hiyo wajumbe wa baraza la wawakilishi wameitaka wizara hiyo kuendelea kutoa elimu katika vyombo vya habari ili viweze kusaidia na kuweza kutokomeza tatizo hilo nchini.
Akitoa majumuuisho waziri kastico amesema bado wazazi wanapaswa kuwa makini na kushirikiana kwa pamoja katika malezi ya watoto wao na sio kuwaachia upande mmoja tu.
Wajumbe wa baraza hilo kwa pamoja wameipitisha hotuba hiyo ya wizara ya kazi uwezeshaji wazee vijana wanawake na watoto.