SERIKALI HAITOMVUMILIA YOYOTE ATAKAEHUSIKA NA UKODISHAJI WA MASHAMBA YA KARAFUU

 

 

Rais wa Zanzibar  na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesema Serikali   haitomvumilia mtu yoyote   atakaehusika na ukodishaji  wa mashamba ya karafuu ya serikali kwa maslahi yake binafsi.

Amesema wako baadhi ya wafanyakazi wa wizara ya kilimo na maaliasili ambao sio waaminifu   wanaotumia mashamba kwa maslahi yao na kuikosesha serikali mapato.

Dk.Shein ameyasema  hayo wakati alipokuwa akizungumza na viongozi wa taasisi  za serikali  pamoja na wakuu wa wilaya  na mkoa katika ukumbi wa makonyo chake chake .

Pia dk Shein amesema serikali imedhamiria  kuongeza kasi ya  usimamizi  wa magendo ya karafuu  ili kudhibiti  upotevu wa karafuu na kuchukua hatua kali  kwa watakaogundulika  kufanya biashara ya magendo

Akizungumzoa suala la wafanyakazi katika taasisi za umma dk. Shein amewataka watendaji wa taasisi  kuwajibika ipasavyo  kwa  kusimamia sera , sheria na  taratibu za utumishi wa umma   ili lengo la kuwahudumia wananchi liweze kufikiwa .

Sambamba na hayo dk. Shein amewataka viongozi  hao kutoliyogomba suala la  ugatunzi wa madaraka  kwani hakuna  kiongozi yoyote atakae  pokonywa madaraka na badala yake  serikali imeiyagiza   wizara husika  kuweza kutowa taaluma  kwa  taasisi zinazohusika kuingia katika  serikali za mitaani.

Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapindunzi dk. Ali Mohammed Shein amewasili  kisiwani pemba kwa  ziara ya siku tano katika kukaguwa   na kufunguwa miradi mbali mbali ya mendeleo.