SERIKALI HAITOVUMILIA VITENDO VYA WAAJIRI WA SEKTA BINAFSI WANAOWANYANYASA WAFANYAKAZI

Serikali ya mapinduzi zanzibar imesema haitovumilia vitendo vya baadhi ya waajiri wa sekta binafsi wanaowanyanyasa wafanyakazi bila ya sababu za msingi.
Naibu wazir iwa kazi, uwezeshaji, wazee, vijana, wanawake na watoto mh. Shadya mohamed suleiman amesema zipo baadhi ya taasisi zimekuwa zikiwanyima haki watumishi wake ikiwemo kuwafukuza, kusitish mikataba bila kufuata sheria.

Amezungumza hayo alipofanya ziara katika hospitali ya global kusikiliza malalamiko ya baadhi ya wafanyakazi kuhusiana na utendaji wao ambapo waziri huyo amefahamisha kuwa serikali imeweka sheria za utendaji wa sekta binafsi na lazima zifuatwe ili kuepusha migogoro ya kiutendaji.
Uongozi wa hospitali hiyo katika maelezo yao kwa naibu waziri umeeleza kuwa unatekeleza majukumu yao inavyotakiwa.
Kwa mujibu wa maelezo ya wafanyakazi wamesema wamekuwa hawana uhakika na ajira zao kutokana na kutoelewa mikataba yao pamoja na kutolipwa mishahara inavyoridhisha.