SERIKALI IMEANDAA MPANGO WA UPEMBUZI YAKINIFU WA KUJENGA UPYA UWANJA NDEGE WA PEMBA

Katika kuimarisha huduma za usafiri wa anga na kukuza uchumi kupitia sekta ya utalii Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeandaa mpango wa upembuzi yakinifu wa kujenga upya uwanja ndege wa Pemba ili kuweza kutoa huduma kama vilivyo viwanja vingine ulimwenguni
Akiwa katika kikao cha pamoja na wataalamu wa mradi huo kutoka kampuni ya DAR ALHANDA kutoka nchini Misri Naibu katibu mkuu wa wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Shomari Omar Shomar amesema kufanikiwa kwa upembuzi huo utasaidia kupata viwanja vyenye ubora na kuongeza kasi ya usafirishaji wa abiria na utalii nchini
Amesema Serikali ya Zanzibar kwa kushirikiana na Serikali ya Muungano imepata mkopo wa kuimarisha sekta ya usafiri wa anga kwa kufanya upembuzi yakinifu kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) ambapo katika mpango huo kutafanyika usanifu wa kina na utayarishaji wa zabuni za ujenzi wa uwanja wa ndege Pemba na utayarishaji mpango mkuu wa viwanja vya ndege vya Zanzibar na utayarishaji wa mpango wa matumizi bora ya ardhi kwenye kiwanja cha ndege cha Abeid Karume kisiwani Unguja.
Afisa mdhamini wa wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Ahmed Moh’d Baucha amesema kulikuwa na kilio kikubwa kwa wasafiri na wawekezaji kwamba kiwanja ni kidogo lakini kupitia mradi huo kiwanja hicho kitakuwa bora na wananchi watafaidika na huduma hizo.
Naye mkurugezi wa mradi huo Khamis Shimel amesema wameamua kushirikiana wataalamu wa ndani katika kupima udongo na mambonde kujua kiwango kinachohitajika
Jumla ya shilingi bilioni nne zinatarajiwa kutumika katika upembuzi wa mradi huo utakaohukuwa muda wa miezi 17