SERIKALI IMEANZA KUTEKELEZA UJENZI WA MRADI WA MTARO WA MAJI BUBUJIKO

 

Serikali ya Mkoa wa Kaskazini Pemba imeanza kutekeleza ujenzi wa mradi wa mtaro wa maji uliopo bubujiko wilaya ya wete ili kuzuia athari mbali mbali za kuenea maji machafu.

Mkuu wa mkoa huo mh. Omar Khamis Othman amesema hatua ni utekelezaji wa agizo la rais wa zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi dk. Ali mohamed shein kutaka mradi huo utekelezwe ili kuondosha kero kwa wananchi.

Mkuu huyo wa mkoa alikuwa katika ukaguzi na ushiriki wa ujenzi wa taifa wa mtaro ambapo amewahimiza wananchi kuunga mkono ili kuhakikisha unakamilika kama ilivyokusudiwa.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya wete abeid juma ali ameiomba serikali na wadau wengine kusaidia uendelezaji wa mradi mradi huo ili uweze kukamilika kwa wakati.

Wananchi wa kijiji cha bubujiko wameushukuru uongozi wa mkoa kwa hatua ya kwanza ya ujenzi huo na kuiomba serikali kuongeza nguvu katika ujenzi huo.