SERIKALI IMEENDELEA KUIMARISHA HUDUMA ZA KIJAMII

Rais wa zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi dr. Ali muhammed shein, amesema serikali imefanikiwa kukusanya jumla ya shilingi bilioni mia tano na nne, mia saba na tisa kwa kipindi cha machi 2016 hadi februari 2017.

amesema mafanikio hayo yaliyoyapatikana katika ukusanyaji wa mapato yametokana na juhudi kubwa zilizochukuliwa na serikali katika kuziba mianya ya uvujaji wa mapato kwa kuweka usimamizi madhubuti na mabadiliko ya mbinu katika ukusanyaji wa mapato na usimamizi wa matumizi.
Akizungumza na watendaji wa vyombo vya habari ikulu mjini zanzibar ikwa ni kutimia mwaka mmoja tokea kiingia madarakani, dr. Amesema hali ya amani na utulivu iliyopo nchini imechangia ongezeko hilo la uchumi kwani wageni kutoka mataifa ya kigeni wameendelea kuingia nchini kwa shuhuli za biashara ya

Aidha dr shein amesema serikali imeendelea kuimarisha huduma za kijamii, katika sekta ya afya, elimu, kilimo na uvuvi na kuimarisha miundombinu ya barabara katila mikoa yote ya unguja na pemba.
Ameongeza kuwa serikali itaendelea kushirikiana na sekta binafsi katika harakati za kimaendeleo ikiwemo ujenzi wa wa miji mipya

Kati ya hizo jumla ya tzs milioni 249,279 zilikusanywa kutoka bodi ya mapato, zanzibar (zrb), mamlaka ya mapatotanzania (tra) ilikusanya jumla ya tzs milioni 200,840 na mapato mengine yasiyo ya kodi yaliyokusanywa ni (makusanyo ya mapato kutoka katika wizara na taasisi za serikali) yalikuwa ni tzs milioni 54,590.

Katika ukusanyaji wa mapato, serikali imekusanya jumla ya tzs milioni 504,709 kwa kipindi cha machi, 2016 hadi februari, 2017; kati ya hizo jumla ya tzs milioni 249,279 zilikusanywa kutoka bodi ya mapato, zanzibar (zrb), mamlaka ya mapatotanzania (tra) ilikusanya jumla ya tzs milioni 200,840 na mapato mengine yasiyo ya kodi yaliyokusanywa ni (makusanyo ya mapato kutoka katika wizara na taasisi za serikali) yalikuwa ni tzs milioni 54,590.
Jambo moja kubwa na la muhimu ambalo tunaendelea kujivunia, ni suala la amani na utulivu katika nchi yetu ambao ndio msingi mkubwa wa maendeleo tunayoendelea kuyapata katika sekta zote.natoa shukrani kwa wananchi na kuwapongeza kwa kutambua umuhimu wa kudumisha amani na mshikamano, hatua ambayo inaiwezesha serikali kutekeleza wajibu wake wa kuwatumikia wananchi kwa ufanisi.

Kadhalika,navipongeza vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vya smt na idara maalum za smz kwa kuhakikisha kuwa wananchi wetu na wageni wanaotembelea nchi yetu, wanaendelea kuwa salama pamoja na mipaka yetu.utulivu tulionao umesaidia kwa kiasi kikubwa kukuza sekta ya biashara na utalii ambavyo ndio sekta kiongozi kwa uchumi wetu.

Kwa ujumla, hali ya amani na utulivu imechangia kwa kiasi kikubwa katika kuimarika kwa uchumi wetu. Katika mwaka 2016, uchumi wetu ulikua kwa asilimia 6.6 na mfumko wa bei ulibakia kuwa wa tarakimu moja, asilimia 5.7.

Katika ukusanyaji wa mapato, serikali imekusanya jumla ya tzs milioni 504,709 kwa kipindi cha machi, 2016 hadi februari, 2017; kati ya hizo jumla ya tzs milioni 249,279 zilikusanywa kutoka bodi ya mapato, zanzibar (zrb), mamlaka ya mapatotanzania (tra) ilikusanya jumla ya tzs milioni 200,840 na mapato mengine yasiyo ya kodi yaliyokusanywa ni (makusanyo ya mapato kutoka katika wizara na taasisi za serikali) yalikuwa ni tzs milioni 54,590.

Mapato hayo ya tzs milioni 504,709 yaliyokusanywa yameongezeka kwa tzs milioni 107,039 ikilinganishwa na mapato yaliyokusanywa kwa kipindi kama hichi cha mwaka uliopita (machi, 2015 hadi februari, 2016). Ongezeko hilo ni sawa na asilimia 26.9 .

Mafanikio haya tuliyoyapata katika kukusanya mapato yanatokana na juhudi kubwa zilizochukuliwa kuziba mianya ya uvujaji wa mapato. Tumeweka usimamizi madhubuti na mabadiliko ya mbinu katika ukusanyaji wa mapato na usimamizi wa matumizi. Uamuzi wetu wa kubana matumizi, kupunguza safari za nje ya nchi na ndani, kuondosha posho kwa kulipia semina, kongamano, kugharamia vyakulawakatiwa mikutano, na kadhalika; umesaidia sana, hapa tulipofika leo.

Serikali imefanikiwa kulipa limbikizo la viinua mgongo jumla ya tzs milioni38,251 kwa wastaafu 2,734, kwa malipo ya miezi 26, kuanzia mwezi wa januari, 2015 hadi oktoba, 2016. Deni lililobaki ni la miezi mitatu (novemba, 2016, disemba, 2016, januari, 2017) kwa wastaafu 287 kwa jumla ya tzs milioni 5,473. Haya ni mafanikio makubwa, ambayo hatujawahi kuyafikia.

Aidha, juhudi zetu za kuimarisha ukusanyaji wa mapato zimetuwesha kutekeleza kwa ufanisi mpango ulioanzishwa na serikali ya mapinduzi ya zanzibar ya awamu ya saba wa kuwalipa pensheni wazee waliotimia miaka 70 bila ya kujali historia ya kazi yao. Mafanikio makubwa zaidi ni kwamba serikali imeweza kukidhi mahitaji ya fedha kwa makusanyo yake ya mapato ya ndani bila kuwepo kwa msaada wa kibajeti. Kutokana na mafanikio hayo, serikali imekamilisha matayarisho ya kuongeza mishahara kutokana na mabadiliko ya kukiongeza kima cha chini cha mshahara kutoka tzs 150,000 hadi kufikia tzs 300,000 katika mwezi wa aprili, 2017. Hata hivyo, serikali itaendelea kuongeza kasi ya kubana mianya ya uvujaji wa mapato na kuwashughulikia ipasavyo wale wote wanaojaribu kukwepa kodi kwa njia mbali mbali ili tuweza kuongeza mapato yetu kila mwaka na tuimarishe utoaji wa huduma kwa wananchi.

Ndugu wahariri na waandishi wa habari,
ukuaji wa uchumi umeiwezesha serikali kuimarisha huduma za jamii, hasa elimu, afya na upatikanaji wa maji safi na salama. Katika kipindi hiki, serikali imeendelea kutoa elimu ya msingi bila ya malipo wala ubaguzi. Katika mwaka 2016, idadi ya skuli imeongezeka kutoka 792 mwaka 2015 hadi 843, sawa na ongezeko la asilimia 7. Serikali imeshakamilisha michoro ya ujenzi wa skuli 9 za ghorofa kwa mkopo wa fedha za benki ya dunia zitakazojengwa katika wilaya ya mjini, magharibi a na b kwa unguja na wilaya zote nne za pemba.

Katika kupanua fursa za elimu, katika mwaka uliopita, serikali imekamilisha ujenzi wa skuli ya sekondari ya kwarara ambayo ina studio ya kisasa ya tv na radio ya kurushia matangazo ya elimu. Skuli hii ni aina ya pekee kwa tanzania. Aidha, kituo cha elimu mbadala kimefunguliwa kwa upande wa pemba pamoja na ufunguzi wa skuli kubwa ya kisasa ya sekondari ya mohamed juma pindua ya mkanyageni. Vile vile,katika miezi michache iliyopita, serikali imejenga skuli ya msingi katika kijiji cha mgonjoni ili kuwaondolea wananchi wa kijiji hicho usumbufu wa kufuata huduma hizo katika maeneo ya mbali. Taarifa ya kutia moyo ni kwamba, katika matokeo ya mtihani wa kidato cha nne ya mwaka jana, kiwango cha wanafunzi cha kufaulu kimeimarika ambapo jumla ya wanafunzi 242 walipata daraja la kwanza. Kiwango hiki hakijawahi kufikia kwa miaka mingi iliyopita.

Elimu ya juu imeimarishwa, wanafunzi wa vyuo vikuu wameongezeka kutoka 6,370 katika mwaka 2015 hadi kufikia 7,303 katika mwishoni mwa mwaka 2016. Mikopo ya elimu ya juu imetolewa kwa wanafunzi 2,655 kwa jumla ya tzs bilioni3.7