SERIKALI IMEKUSUDIA KUANZISHA VIWANDA NA KUBUNI MIRADI ITAKAYOWASAIDIA VIJANA

 

 

Naibu spika wa baraza lawawakilishi mh mgeni  hassan juma, amesema serikali imekusudia kuanzisha viwanda  na kubuni miradi itakayowasaidia vijana na waweze kujiajiri  wenyewe bila ya kutegemea ajira kutoka serikalini  pekee.

Amesema vijana wengi wamekuwa wakikabiliwa na ukosefu wa ajira, hivyo kupitia viwanda vitakavyojengwa vitaweza kupunguza tatizo hilo na kuwataka  kutokata tamaa na kutoshawishiwa kujiingiza katika vitendo viovu.Aidha amewasisitiza jumuiya ya wanasheria wanawake[ zafela] kuzidi kuhamasisha vijana  kwa kutoa elimu itakayowasaidia kuwa na maamuzi mema yatakayowasaidia katika maisha yao.

Mjumbewa bodi ya mitandao ya  asasi za kiraiya mkoa kaskazini  ndugu ali omar makame, amewasihi vijana  kujitokeza kwa wingi katika tamasha hilo ili kuitumia vyema fursa za elimu zitakazotolewa kwa kuelimishwa haki zao ambazo hawazitambui.Naye mjummbe wa bodi ya zafela bi fatma gharib, amesema vijana ndio tegemeo katika taifa, hivyo wanalazimika  kubadilika kwa kuchukua juhudi  za kuleta maendeleo yao  kuwa na viongozi imara na makini.