SERIKALI IMESHAURIWA KUCHUKUWA HATUA WATENDAJI WOTE WANAOKIUKA MATAKWA YA SHERIA

 

 

serikali imeshauriwa kuchukuwa hatua watendaji wote wanaokiuka matakwa ya sheria zilizopo kwa maslahi yao binafsi na kulitia hasara taifa.

rai hiyo imetolewa katika ripoti  ya kamati ya kuchunguza na kudhibiti hesabu za serikali na mashirika ya umma pca iliowasilishwa katika baraza la wawakilishi kwa mwaka      2016  – 2017.

mwenyekiti wa  kamati hiyo miraji khamis amesema kitendo cha serikali kuendelea kuwa na muhali kwa watendaji wanaopoteza fedha za umma kinadhoofisha uchumi wa nchi na kuifanya nchi kuwa tegemezi.

ripoti hiyo imebainisha kuwa ili bajeti ya serikali inayoidhinishwa iwe na tija ni lazim a kwa serikali kusimamia vianzio vya mapato yake pamoja na nidhamu ya matumizi ya fedha za umma.

baadhi ya wawakilishi waliochangia ripoti hiyo wakaisisitiza serikali kusisitiza uwazi katika kudhibiti mapato mbali  na kuchungwa fedha za umma pia upo umuhimu wa kufanya uhakiki wa mali za serikalikila mwaka.