SERIKALI IMESITISHA UCHAPISHAJI NA USAMBAJI WA GAZETI LA MWANAHARISI KWA KIPINDI CHA MIEZI 24

Serikali imesitisha uchapishaji na usambaji wa gazeti la kila wiki la mwanaharisi kwa kipindi cha miezi ishirini na minne 24 kutokana na gazeti hilo kukiuka maadili , misingi na sheria za taaluma ya uandishi wa habari.
Akizungumza na waandishi wa habari mkurugenzi idara ya habari maelezo na msemaji mkuu wa serikali dkt hassan abas amesema uamuzi huo umechukuliwa kwa mujibu wa kifungu cha 59 cha sheria ya huduma za habari na 12 ya mwaka 2017 kwa kuziingatia kuwa serikali kupitia idara ya habari maelezo ilifanya jitihada za juwakumbusha wahariri wa gazeti hilo juu ya wajibu wa kufuata misingi ya taaluma bila mafanikio.
Ameelezea baadhi ya habari zilizochapishwa na gazeti hilo kwa kukiuka maadili misingi na kujikita katika uchochezi au kusababisha hatari kwa usalama wa taifa.
Aidha dkt abas amesema mnamo tarehe 17 hadi 23 ya mwezi april 2017 gazeti hilo katika toleo lake namba 387 lilichapisha habari iliyosomeka “mwakyembe:maisha yangu yako hatarini” ambapo pia tarehe 4 hadi 10 ya mwezi septemba 2017 gazeti hilo likachapisha habari ilosomeka “makinikia yakwama, na licha ya kuelezwa juu ya udhaifu huo uongozi wa mwanaharishi ulikataa kuomba radhi.
Dkt abas akatumia fursa hiyo kuvikumbusha vyombo vya habari na wanahabari juu ya umuhimi wa kufuata sheria na kanuni zinazoongoza kada hiyo.