SERIKALI IMETANGAZA MAJINA YA MASHEHA WAPYA WATAKAOSIMAMAIA SHEHIA MBALI MBALI

 

 

 

 

Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mh Ayoub Mohamed Mahmoud amewataka masheha kutoa huduma kwa jamii kwa kuzingatia miongozo ya majukumu yao na kuacha kuyumbishwa na wanasiasa.

amesema dhamira ya mkoa huo ni kuhakikisha wananchi  wanasaidiwa kupata huduma bora hali itakatakayoondosha malalamiko katika shehia zao na kufanikisha  mkoa huo kuwa na amani na utulivu.

akizungumza na masheha wapya wa shehia za mkoa huo Mh Ayoub amesema mabadiliko ya serikali za mitaa imeleta mageuzi makubwa ya utendaji kwa viongozi hao hivyo wanapaswa kuwa tayari kukabiliana na mabadiliko hayo kwa kufanya kazi bila ya woga

Mh Ayoub amewasisitiza kuweka mikakati ya kukabiliana na matatizo mbalimbali yaliyomo katika shehia zao ikiwemo migogoro ya ardhi na dawa  za kulevya na uhalifu.

wakuu wa wilaya za mkoa huo pamoja na Kamanda wa Polisi Mkoa Mjini Magharibi Hassan Nassir wametoa nasaha zao kwa masheha hao na kuwasititiza kushirikiana na viongozi hao.

baadhi ya Masheha wameeleza namna watakapofanya kazi katika Shehia zao

Masheha hao walikula kiapo cha utii na uadilifu kwa ajili ya kutumikia nafasi hizo.