SERIKALI IMEWEKA MKAKATI WA KUTAFUTA NJIA NYINGINE ZA KUPATA UMEME

 

Naibu katibu mkuu wizara ya ardhi maji nishati na mazingira ndugu tahir abdalla  amesema serikali imeweka mkakati wa kutafuta njia nyingine za kupata umeme ili kuhakikisha inakuwa na nashati ya kutosheleza  mahitaji ya sasa na baadae.

Amesema visiwa vya unguja na pemba vinakuwa kimaendeleo kila kukicha kutokana na kuimarika mradi ya kiuchumi, hivyo kujiimarisha kwa kiwango kikubwa cha umeme ni jambo la lazima.

Akifunguwa semina elekezi juu ya nishati kwa wanafunzi wa skuli mbali mbali za unguja katika kituo cha elimu mbadala rahaleo mjini zanzibar, ndugu tahir amesema katika kufanikisha mkakati huo serikali kwa kushirikaana na wadau wa maendeleo inaendelea kufanya utafiti juu ya upatikanaji wa umeme huo ili isitegemee umeme kutoka tanzania bara pekee.

Amewataka  wanafunzi wanaoshiriki semina hiyo  ambao pia wanajishughulisha na masuala ya mazingira kuitumia nafasi hiyo kuisaidia serikali katika kuiwezesha zanzibar kuwa na umeme wake mwenyewe na utakaokidhi mahitaji.

Kaimu  mkurugenzi idara ya nishati zanzibar  ndugu omar saleh mohammed amesema utafiti uliofanywa kupitia minaza maalum iliyojengwa makaunduchi,matemwe na nungwi kwa unguja na micheweni na mwambe kisiwani pemba umeonesha zanzibar ina uwezo wa kuwa na umeme wa kutosha unaotokana na jua.

Afisa wa mradi wa nishati rafiki ndugu sebastian sanga amesema wakati umefika wa kuhakikisha nishati ya umeme imefika katika maeneo yote ya zanzibar na kila mwananchi anautumia.

Afisa kutoka wizara ya elimu na mafunzo ya amali ndugu suhuba daudi issa amesema serikali imefikiria jambo la maana kuwashirikisha wanafunzi waskuli katika utafiti wa upatikanaji wa nishati kwa vile ni taifa la kesho na  wana wafasi kubwa ya kuelimsha jamii.