SERIKALI INAENDELEA JITIHADA ZA KUWAPATIA MISAADA ZAIDI.WAATHIRIKA WA MVUA

mkuu wa wilaya ya kati Nd Mashavu Sukwa  amesema  serikali inaendelea  na tathmini ya athari za mvua na maafa yaliyawafika wananchi na jitihada za kuwapatia misaada zaidi.

nd mashavu ametoa kauli hiyo wakati akikabidhi zaidi ya shilling million mbili zilizotolewa na serikali kusaidia waathirika wa mvua hizo kutoka shehia mbalimbali za wilaya ya kati.

aidha nd sukwa  amewataka wananchi hao kuwa wastahamilivu na kwamba serikali inakamilisha taratibu za tathmini za maafa ili iweze kuwapatia misaada kulingana na maafa yaliyowakuta.

wakipokea msaada huo katika ofisi ya mkuu wa wilaya ya kati dunga wananchi hao wamesema wameishukuru serikali kwa juhudi za kuwapatia misaada hiyo ikiwemo chakula n fedha taslim.

jumla ya wananchi  hamsini na tatu kutoka wilaya ya kati waliopatwa na maafa ya kuingia maji nyumba zao wamepatiwa msaada huo.