SERIKALI INAENDELEA NA AZMA YAKE YA KUKAMILISHA MRADI WA UTAFITI WA NISHATI MBADALA

Serikali  inaendelea  na azma yake  ya  kukamilisha  mradi  wa utafiti  wa  nishati  mbadala   ili  kujua  uwezekano  wa  Zanzibar   kupata  umeme  kwa  njia  mbadala.

akiwasilisha  hotuba  ya  makadirio na  mapato  ya  mwaka  2017/2018   waziri  wa  ardhi  maji  nishati  na  mazingira  waziri  wa  wizara  hiyo  Mh  Salama  Aboud  amesema  takwimu  zinazoendelea  kukusanywa   zinaashiria  uwezekano  mzuri  wa   wa  matumizi  ya  nishati   mbadala  kwa  zanzibar.

amesema  kazi  za  utafiti   zinaendeshwa  na  kampuni  ya  mwh  ya Ubelgiji  ambapo  inatarajia  kukamilisha  kazi  zake   mwezi  juni  mwakani  ambapo  nchi  itakuwa  na  mazingira  bora  ya  uwekezaji wa  nishati  mbadala.

akizungumzia  kuhusu  ukusanyaji  wa  mapato  kwa  uchandgiaji  wa  huduma  ya  maji  hawakuweza   kufikia  malengo  kutokana na  baadhi  ya  maeneo  kuwa  na  upungufu  wa  maji    pamoja  na  wananchi  kukosa  mwamko  wa   kuchangia  huduma  hiyo.

akiwasilisha  maoni  ya  kamati  y a ardhi  na  mawasiliano   Mh  Hamza  Hassan  Juma  wameiomba  wizara  kushirikiana  na  afisi  ya  mwanasheria  Mkuu wa  Serikali   pamoja  na  tume  ya  kurekebisha  sheria   zinazohusiana  na masuala  mtambuka  ya  ardhi   ambazo  husababisha   kuongezeka  migogoro  ya  ardhi  nchini.