SERIKALI INAKUSUDIA KUONGEZA UZALISHAJI WA MAZAO MENGINE KUPITIA MALIGHAFI ZA MIKARAFUU

 

 

 

Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko Balozi Amina Salum Ali amesema serikali amesema serikali inakusudia kuongeza uzalishaji wa mazao mengine kupitia malighafi za mkarafuu ili zao hilo liwasaidie wananchi katika harakati za kimaisha bila ya kubabaika.

Amesema uongezaji wa thamani wa malighafi za mkarafuu ni wa kiwango cha chini na haujamnufaisha mwananchi wa kawaida, kwani kwa sasa zaidi huzalisha mafuta ya makonyo ambayo uzalishaje wake ni mdogo na haukidhi majitahi ya soko husika.Balozi Amina ametowa kauli hiyo kiwanda cha Makonyo wakati akifungua kikao cha kujadili matokeo ya uwokowaji wa zao la kafaruu katika msimu unaomaliza kilichowashirikisha masheha, wajumbe wa kamati za ulinzi na usalama wa wilaya Mkoa wa Kusini na watendaji wa taasisi za serikali.

Amesema muelekeo wizara hiyo ni mkarafuu na maisha ya mzanzibar kwani karafuu ni zao pekee linalowakombo wananchi mmoja mmoja na taifa katika shughuli za za kiuchumi.Akizungumzia suala la uokowaji wa zao hilo Balozi Amina ameanza kwa kutowa shukrani kwa utaratibu wa ulinzi wa karafuu uliofanywa katika msimu unaomalizika kwani umetowa heshima kwa SMZ katika kudhibiti zao la kafaruu.Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mh. Hemed Suleiman Abdalla amesema ingawa msimu wa kuvuna karafuu umemalizika, lakini mkoa wa Kusini hautokubali kuona zao hilo li natumika kinyume na sheria.