SERIKALI INAYAFANYIA KAZI MALALAMIKO YA WAFANYABIASHARA WANAODAI KULIPA KODI MARA MBILI

 

Waziri wa nchi ofisi wa makamu wa rais anayeshughulikia muungano na mazingira January Makamba amesema serikali inayafanyia kazi malalamiko ya wafanyabiashara wanaodai kulipa kodi mara mbili ili kuiimarisha sekta hito tegemeo kwa uchumi wa nchi.

akizungumza wakati wa ziara ya kutembelea tra na zrb na bandari ya malindi amesema atajitahidi kuyashughulikia masula yanayoutia dosari muungano  yakiwemo ya biashara yasihatarishe kuvunjika kwa muungano huo.

Amesema  kwa muda mrefu wafanya biasha wa  zanzibar wamekuwa wakilalamika kulipishwaji wa kodi mara mbili jambo ambao kama linaukweli ni lazima lifanyiwe ufumbuzi.

Kwa upande wa  wa mamlaka ya mapato tanzania (tra) wamesema   wanafuata vizuri taratibu zilizounda za ukusanyaji wa mapato lakini  zrb  hulipishwa  mzigo mara mbili baada ya  wafanya biashara  kulipa bandar ya dar es salaam.

Naye mkurungezi wa bandar ya unguja ndugu  abdala juma abdala amesema kumekuwa na changamoto   kuhusu  masuala ya bandarini  ambapo  shirikala bandari zanzibar linawadai  fedha  zaidi ya biioni  mbili  bandari tanzania bara .

Aidha amefahamisha kwamba kuna bandari bubu zipatazo hamsini unguja na pemba ambazo zinadaiwa kusafirisha magendo na kuikosesha serikali mapato.