SERIKALI INAZINGATIA MAHITAJI YA UPATIKANAJI WA ELIMU KATIKA MAZINGIRA BORA

Waziri wa elimu na mafunzo ya amali mh. Riziki pembe juma amesema serikali inazingatia mahitaji ya upatikanaji wa elimu katika mazingira bora na kwa urahisi ili kupunguza adha ya watoto kutembea masafa ya mbali kufuata elimu.
Akizungumza wakati alipokagua maendelo ya ujenzi wa skuli ya msingi na sekondari pangawe mh. Riziki amesema kukamilika kwa ujenzi huo mwezi marchi mwakani utatoa fursa ya wanafunzi wa maeneo jirani kuitumia skuli hiyo kinyume na ilivyo sasa kusoma skuli za mbali.
Hata hivyo waziri wa elimu amesema ni matarajio yaserikali kuona skuli hiyo inamalizika kabla ya mwezi marchi ili wanafunzi waanze kuitumia katika mwaka mpya wa masomo.
Mhandisi wa ujenzi huo kutoka wizara ya elimu said shaaban amesema mradi wa skuli hiyo yenye madarasa 20 utagharimu dola milioni nne ikiwa ni ufadhili kutoka serikali ya china umezingatia vigezo vya watu wenye mahitaji maalum ili wapate fursa sawa ya elimu kama watoto wengine.