SERIKALI ITAAJIRI MAFUNDI MITAMBO ISHIRINI KATIKA SHIRIKA LA UTANGAZAJI ZANZIBAR

Waziri wa habari utalii utamaduni na michezo mhe rashid ali juma amesema serikali itaajiri mafundi mitambo ishirini katika shirika la utangazaji zanzibar watakaojaza nafasi za waliostaafu na wengine wanaotarajiwea kustaafu hivi karibuni.
Akijibu hoja za wajumbe mbali mbali wa baraza la wawakilishi waliochangia taarifa ya utekelezaji wa wizara hiyo katika kikao cha baraza la wawakilishi kinachoendelea hivi sasa, waziri rashidf amesema serikali imeweka kipaumbele kuimarisha shirika la utangazaji zbc ili limudu ushindani na vyombo vingine vya habari hivyo uajiri wa mafundi hao ni sehemu ya mikakati hiyo.
Aidha amesema wizara imejizatiti kuimarisha ukusanyaji wa mapato kwa njia za kisasa kabisa katika vianzio vyake mbali mbali yakiwemo maeneo ya historia ili kuepusha udanganyifu unaosababisha upotevu wa fedha.