SERIKALI ITAENDELEA KUIMARISHA HUDUMA ZA JAMII IKIWEMO AFYA BORA

Serikali itaendelea kuimarisha huduma za jamii ikiwemo afya bora ili kwenda sambamba na azma ya mapinduzi ya zanzibar .
Waziri wa nchi ofisi ya raisi , tawala za mikoa , serikali za mitaa na idara malum za smz mh’ haji omar kheri katika hafla ya uzinduzi wa wodi ya wazazi sebleni katika mkoa wa mjini magha ribi.
Amepongeza juhudi za bodi ya afya na kuwataka akina baba kujenga utamaduni wa kuwa karibu na wake zao wanapokuwa wajawazito katika suala zima la kufatilia huduma za afya ili kuepusha athari zinazoweza kujitokeza kabla na baada ya kujifungua .
Mkuuu wa mkoa mjini magharibi mh; ayoub mohammed mah’moud ameahidi kuongeza ushirikiano na wizara ya afya kuweka mikakati ya huduma bora.
Nae mkurugenzi mkuu wizara ya afya dkt. Jamala adam taib amesema serikali itaongeza vituo vya afya vitakavyotoa huduma mbali mbali ili kuepusha usumbufu kwa wananchi kwa kufaidika na huduma za afya.