SERIKALI ITAENDELEA KUIMARISHA MAENDELEO KWA KUSHIRIKIANA NA WADAU MBALIMBALI.

 

Mkuu wa mkoa mjini magharibi mh. Ayoub mohammed mahmoud amesema serikali ya mkoa huo itaendelea kuimarisha maendeleo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.

Amesema wajibu wa serikali ni  kusaidia maendeleo ya wananchi  wake na kuwatengenezea mazingira mazuri ya kuendesha maisha yao na kuwapunguzia ukali wa maisha yao ya kila siku.

Mhe ayoub ameeleza hayo hapo ofisini kwake vuga katika hafla maaalum ya kukabidhi  computer zilizotolewa na mfanyabiashara  said salim bopar na kuzikabidhi kwa wenyeviti wachama  cha  mapinduzi mkoa wa mjini kichama ,mkoa wa magharibi na uongozi wa skuli ya  sos.

Aidha mkuu wa mkoa amesema ataendelea kushirikiana na viongozi na  wanachama  wa chama cha  mapinduzi katika kuzitumia vyema fursa ziliopo katika mkoa  wake ili kuona chama hicho kinaendelea kuwa na mazingira bora

Kwa ngazi mbalimbali      sambamba na kuhakikisha anatekelezaa hadi zake kwa wakati hususani katika sekta ya elimu.

Mapema akizungumza  katika ghafla hiyo mfanyabiashara nd said salim bopar amesema amekuwa na utaratibu maalum kutoa sehemu ya faida anayoipata katika biashara kwa kusaidia shughuli za kijamii yakiwemo makundi maalum kwa azma ya  kuunga mkono juhudi zinazochukuliwa na serikali katika kuwahudumia wananchi.

Wakitoa shukran imara baada ya kupokea msaada wa  computer  mwalimu mkuu wa skuli ya  sos  na  wenyeviti   wa chama cha mapinduzi   mkoa  wa  mjini na magharibi  kichama  wamepongeza  juhud i zinazochukuliwa  na   uongoz i wa mkoa   mjini magharibi  katika  kusimamia  vyema  maendeleo  ya  mko a huo pamoja na mashirikano makubwa wanayoyatoa katika taasisi na sekta mbalimbali  seikali na watu binafsi .

Computer saba ( 7 ) zimekabidhawa ambapo tano zimetolewa kwa uongozi  wa skuli ya sos kufuati aahadi iliyotolewa hivi karibun i na mhe mkuu wa mkoa na mbili  kwa uongozi wa mkoa wa mjini kichama .