SERIKALI ITAENDELEA KUIMARISHA UTAWALA BORA UNAOZINGATIA SHERIA

 

Makamu wa rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania muheshimiwa samia suluhu hassan amesema  serikali itaendelea kuimarisha utawala bora unaozingatia sheria ili kila raia wa nchi hii aishi kwa amani na utulivi huku ikitoa ruhusa kwa kila mmoja kuekeza katika miradi ya maendeleo.Muheshimiwa samia amesema hayo  wakati akizungumza na  askari polisi pamoja na wananchi  mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika  nyumba za maakaazi ya askari wa jeshi hilo huko mfikiwa mkoa wa kusini pemba.

Amesema utawala bora ndio msingi  wa amani na utulivu katika nchi hivyo  amewataka wananchi  kuheshimu utawala wa sheria na kushirikiana na jeshi la polisi katika kutoa taarifa za uvunjifu  wa amani pindi itakapotoea ili kuona amani iliopo inaendelea kudumu.Katika hatua nyengine muheshimiwa samia amepongeza ujuenzi wa nyumba za makaazi ya polisi na kusema kuwa uwepo wa makaazi mema ndio njia moja wapo ya kuwafanya askari hao kutimiza majukumu yao ya ulinzi wa raia na mali zao kwa ufanisi.

Wakati huo huo muheshimiwa samia ameipongeza kampuni ya tanga sement  na kampuni ya subash patel  kwa msaada wao katika ujenzi wa nyumba za  makaazi ya askari polisi kisiwani pemba.Kwa upande wake inspecta general wa polisi tanzania  saimon siro  amesema    jeshi la polisi limeanzisha  mpango endelevu  wa kuanzisha ujenzi wa nyumba za askari ili kuhakikisha wanaishi katika makaazi bora.Jumla ya nyumba  36 za makaazi ya askari wa jeshi la polisi kisiwani pemba zinatarajiwa kujengwa ambapo katika mkoa wa kusini pemba zitajengwa nyumba 24 na 12 katika mkoa wa kaskazini pemba.