SERIKALI ITAENDELEA KUSIMAMIA MATUMIZI YA RASILIMALI YA ARDHI

Waziri wa wizara ya kilimo, maliasili, mifugo na uvuvi Mh.Hamad Rashid Mohammed amesema serikali itaendelea kusimamia matumizi ya rasilimali ya ardhi ili kulinda maeneo ya kilimo yasichimbwe mchanga.
Amesema matumizi ya rasilimali hizo ikiwemo mchanga inaonekana kuendelea kutumika vibaya ambapo kunasababisha kutokea uharibifu wa mazingira.
Kauli hiyo imetolewa na waziri wa kilimo,maliasili,mifugo na uvuvi mh.hamad rashid muhammed wakati alipokuwa akizungumza na viongozi wa mikoa na wilaya pamoja na wadau wa mchanga huko katika ukumbi wa kiwanda cha makonyo wawi.
Mh.waziri amesema serikali haina adhma ya kufanya biashara ya mchanga wala kuwanyanganya wananchi maeneo yao bali serikali ndio msimamizi mkuu wa ardhi kwa kuweza kupanga mipangili yake kwa kuepusha mazara ya nayoweza kutokea pamoja na kuona rasilimali ya mchanga ilioyopo inakuwa endelevu huku akiwataka viongozi hao kuweza kusimamia bei elekezi ya uchimbaji wa rasilimali hiyo kwa mujibu wa sheria.
Nae mkuu wa mkoa wa kusini pemba mh. Mwanajuma majidi abdalla mapema akizungumza katika mkutano huo aliwataka viongozi wenzake kusimamia kwa vitendo maagizo yanayotolewa na serikali. Nao wadau wa mkutano huo wameitaka serikali kuweza kuwashirikisha walengwa wakati wanapopanga mipango yao ili kuweza kuondosha mivutano baina yao na serikali.
Sambamba na hayo mh.waziri ametembelea eneo la msitu wa hifadhi ngezi vumawimbi ambapo eneo hilo linaonekana baadhi ya watu kujimilikisha kinyume na sheria huku akiitaka idara husika kuondosha alama za vipimo zilizowekwa katika eneo hilo la hifadhi.